Pata shika la nguo kuchaika kati ya ffu wa ngoma africa band na washabiki sugu mjini Frankfurt,
katika onyesho ambalo washabiki walionyesha ubabe dhidi ya walinzi na kulikwea
jukwaa baada ya kudatatishwa na mdundo wa Ngoma Africa band aka FFU.
Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja alikiongoza jukwaani kikosi chake
ambacho mshambuliaji wa gitaa la solo Chris-B aka "Mshenzi" wa gitaa,alikua akipereka
makombora mazito ya milio ya nyuki katika gitaa. Safu ya washambuliaji wa mbele
ikiongozwa na kamanda ras makunja,akiwemo Diva Princess Bedi Beraca bella,
ilikua na kazi ya moja tu..nayo kushambuliana jino kwa jino na washabiki,
Washabiki nao walipopandisha mzuka wao wa mziki walirudisha mashambulizi ndani
ya ulingo wa dansi ! si watoto wala wakubwa,wanawake kwa wanaume! wazungu na weusi
wote wamedata akili mbele ya mziki wa ngoma africa band aka FFU,onyesho la jumamosi
6.08.2011 kule frankfurt Ujerumani.
wasikilize zaidi FFU at www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment