Tuesday, February 22, 2011
Tetemeko la ardhi laikumba New Zealand
Tetemeko la ardhi lililo katika kipimo cha 6.3 ambalo limeukumba mji wa Christchurch nchini New Zealand leo ni moja kati ya matetemeko mabaya sana kuwahi kutokea nchi humo tangu kuanza kuhifadhi takwimu.
Tetemeko hilo lilitokea majira ya mchana kwa saa za New Zealand, na lilitokea katika eneo kilometa tano kaskazini magharibi ya mji wa Christchurch, kwa mujibu wa uchunguzi wa taasisi ya masuala ya ardhi nchini Marekani. Tetemeko hilo lilifuatiwa na matetemeko mengine yaliyofikia katika kipimo cha 5.6.
Meya wa mji wa Christchurch ametangaza hali ya hatari leo Jumanne, akisema kuwa ni siku mbaya kwa mji huo uliokumbwa na tetemeko nchini New Zealand.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment