Tuesday, February 22, 2011

Merkel akiri kushindwa Hamburg


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekiri kile alichokiita kushindwa vibaya, uchaguzi katika jimbo la mji wa Hamburg. Chama cha Christian Democratic Union cha Merkel kimetupwa nje katika uchaguzi uliofanyika katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ujerumani, kikiporomoka kwa asilimia 20 kutoka uchaguzi uliopita na kujikingia kiasi cha asilimia 21.9 tu ya kura. Chama cha upinzani cha Social Democrats, kikiongozwa na waziri wa zamani wa kazi Olaf Scholz, kimenyakua asilimia 48.3, na kukiwezesha chama hicho kutawala peke yake katika jimbo hilo la hamburg. Merkel amesema kipigo hicho kimesababishwa na masuala ya ndani, lakini kushindwa huko kuna maana kuwa chama chake kitapoteza viti vitatu zaidi katika baraza la wawakilishi wa majimbo, Bundesrat, na kufanya kuwa vigumu kupitisha miswada bungeni. Huo ni uchaguzi wa kwanza kati ya chaguzi saba za majimbo zitakazofanyika nchini Ujerumani mwaka huu.

No comments:

Post a Comment