Wananchi waliwapongeza wanajeshi kwa kuungana na mapinduzi wakiendelea kudai kuondolewa kwa wanachama wa chama tawala cha zamani cha RCD
Polisi huko Tunisia wamewaweka washirika wakuu wawili wa rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali kwenye kifungo cha nyumbani, na kumkamata mmiliki wa kituo kimoja binafsi ambae anauhusiano na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani.
Vyombo vya habari vya serikali viliripoti Jumapili kwamba, Larbi Nasra, mmiliki wa Hannibal TV, na jama yake mke wa rais wa zamani Ben Ali, alikamatwa kwa madai ya uhaini.
Watu wengine waliokamatwa walikuwa msemaji wa rais wa zamani Abdelaziz Ben Dhia na mkuu wa baraza la Seneti Abdallah Kallel.
Wakati huo huo wanadamanaji waliendelea kudai kuondolewa kila mtu aliyehusika au kushiriki katika utawala wa rais wa zamani aliyekimbia nchi mapema mwezi huu. Mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Tunis Jumapili hadi wakati wa usiku wakidai kwamba mawaziri na maafisa wote walokua katika utawala wa Ben Ali wasihusishwe na serikali mpya.
wandamanaji walikusanyika usiku mzima mbele ya afisi ya waziri mkuu kumtaka kaimu rais na waziri mkuu walokuwa katika serikali iliyoondoelwa,
Waathirika wa ukame Somalia waelekea Mogadishu
Kufuatia uhaba mkubwa wa chakula uliosababishwa na ukame, idadi kubwa ya wenye mifugo Somalia wanaelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema ukame unazidi kuwa mbaya katika eneo la kusini magharibi la Gedo ambapo wakaazi wanahitaji misaada ya dharura ya maji, chakula na dawa. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema watu wengi wameyakimbia maeneo la Kati na Chini mwa Shebele na wanawasili Mogadishu kila siku. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni yale yanayopakana na kaskazini mashariki mwa Kenya na kusini Mashariki mwa Ethiopia kama vile Wanlaweyne, Toro-torow, Furuqleey, Farsooleey na Dugulle katika jimbo Shabelle. Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani linasema takribani Wasomali milioni mbili na nusu wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.
Saturday, January 22, 2011
Muigizaji Clooney apata malaria Sudan
George Clooney
Muigizaji wa Hollywood George Clooney alipata malaria alipotembelea Sudan mapema mwezi huu, lakini kwa sasa amepona.
Clooney mwenye umri wa miaka 49 hutembelea mara kwa mara nchi hiyo iliyopo barani Afrika kwa ajili ya kueneza zaidi taarifa za eneo lenye mgogoro la Darfur.
Alisema kwa uzoefu wake binafsi imeonyesha kuwa dawa muafaka inaweza kubadili "hali mbaya inayoweza hata kuua" na kuwa "siku 10 ambazo si nzuri badala ya kifo."
Msemaji wake Stan Rosenfield alisema hii ni mara ya pili kwa Clooney kupata maradhi hayo.
Muigizaji huyo anatarajiwa kujadili hali yake hiyo na kazi yake barani Afrika katika kipindi cha Piers Morgan cha CNN siku ya Ijumaa.
Afisa wa Congo akamatwa juu ya ubakaji
Maafisa na Umoja wa Mataifa umesema, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemkamata afisa wa jeshi juu ya tuhuma za ubakaji wa raia wengi uliofanyika Januari 1 mashariki mwa nchi hiyo.
Lt Kanali Kibibi Mutware anashutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa zaidi ya wanawake 50 huko Fizi, jimbo la Kivu ya kaskazini.
Kanali Kibibi ameyatupilia madai hayo na kusema ni uvumi.
Kumekuwa na matukio mengi ya ubakaji wa wanawake wengi mashariki mwa Congo, lakini hili limekuwa tukio kubwa la mara moja kutokea ambalo limehusisha jeshi.
Tahirou Diao, msemaji wa umoja wa mataifa huko Uvira karibu na Fizi, alisema maafisa wa kijeshi wa Congo walimkamata walipotembelea Fizi.
Wanawake wa Congo wakipinga ubakaji
Maso'a Mwenembuka, mkuu wa manispaa ya Fizi, alithibitisha kumwona Kanali Kibibi akiwa amefungwa pingu na kuondoshwa, pamoja na takriban wanajeshi wengine 10 waliokamatwa wakihusishwa na ghasia hizo zilizotokea siku ya mwaka mpya.
Vyanzo vya kijeshi na mashirika ya kutetea haki za binadamu vimesema matukio hayo ya mwaka mpya yalianza wakati kundi la watu lilipomvamia askari ambaye alimpiga risasi raia- ikidaiwa kuwa walikuwa wakigombania mwanamke.
Baada ya hapo kundi la wanajeshi likaamua kulipiza kisasi kwa watu wa Fizi.
Ofisi ya umoja wa mataifa ilisema wanajeshi waliwapiga kisu watu 26, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka minne, kuharibu zaidi ya nyumba 200 na kubaka idadi kubwa ya wanawake.
Wakaazi wengi wa Fizi na muathirika wa madai hayo ya ubakaji wameshutumu Kanali Kibibi, afisa kamanda wa eneo hilo, kwa kuongoza vurugu hizo.
Lakini katika mahojiano na BBC wiki hii, alikana madai hayo na kusema wanajeshi waliofanya uhalifu huo walikiuka amri yake.
Ghasia za miaka 16 mashariki mwa Congo zimekithiri kwa udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike.
Zaidi ya wanawake 300, wanaume na watoto walibakwa na muungano wa makundi ya waasi katika mji wa Luvungi na vijiji jirani kaskazini mwa Kivu kilomita kadhaa kutoka kituo cha umoja wa mataifa mwezi Agosti.
Wananchi wa Gaza waonyesha hasira zao mbele ya Waziri wa Ufaransa
Wapalestina wameandamana kupinga safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa kwenye Ukanda wa Gaza unaoendelewa kuzingirwa kila upande na utawala dhalimu wa Kizayuni. Waandamanaji hao wenye hasira walijitahidi kuzuia gari lililokuwa limembeba Bi. Michèle Alliot-Marie Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa lisivuke mpaka wa Gaza na kuingia katika eneo hilo. Miongoni mwa waandamanaji hao walikuwa ni familia za wafungwa wa Palestina walioko katika jela za kutisha za Israel ambao wamesema kuwa, safari ya Alliot-Marie ina lengo la kufuatilia misimamo yenye kuipendelea serikali ya Tel Aviv na wamemshutumu kuwa anapuuza jinai za kivita zinazoendelea kutendwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina. Kabla ya kuelekea Gaza, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa alikutana na baba wa Gilat Shalit askari Mzayuni anayeshikiliwa mateka na harakati ya Hamas katika Ukanda wa Gaza. Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amepuuza jinai za Wazayuni na badala yake kuilaumu harakati ya HAMAS kwa kumshikilia mateka askari wa Israel wakati utawala wa Kizayuni wenyewe unaendelea kuwashikilia mateka mamia ya Wapalestina na kufanya jinai kubwa dhidi yao.
Odinga asema, wanapoteza fursa kuhusiana na Ivory Coast
Raila Odinga Waziri Mkuu wa Kenya ambaye ameshindwa kupatanisha mgogoro wa Ivory Coast amesema kuwa wanapoteza fursa za kutatua mgogoro wa nchi hiyo. Odinga ameongeza kuwa, si vyema kuufunga haraka mlango wa mazungumo na kwamba wataendelea kujitahidi kutafuta suluhisho la amani. Aidha amesema chaguo la kutumiwa nguvu za kijeshi bado lipo lakini ni la mwisho na litatekelewa iwapo jitihada nyinginezo zitashindikana. Laurent Gbagbo rais anayeng'anga'nia madarakani nchini Ivory Coast amekataa wito wa jamii ya kimataifa wa kuondoka madarakani kwa amani na kumkabidhi uongozi wa nchi hasimu wake Alassane Ouatta ambaye ameshinda uchaguzi wa rais wa Novemba 28 nchini humo.
Friday, January 21, 2011
Majeshi ya magharibi mwa Afrika yako tayari kuingia Ivory Coast
Majeshi ya nchi za magharibi mwa Afika yametangaza kuwa yako tayari kuingilia kijeshi nchini Ivory Coast. Jenerali Mnigeria Olusegun Petinrin amesema baada ya kikao cha makamanda wa jeshi wa nchi za magharibi mwa Afrika waliokutana jana mjini Bamako Mali kwamba vikosi vya majeshi ya nchi za eneo hilo viko tayari kutumwa nchini Ivory Coast. Jenerali Petinrin amesema vikosi vya majeshi ya ECOMOG vinasubiri amri ya marais wa nchi za magharibi mwa Afrika kwa ajili ya kuingilia kijeshi huko Ivory Coast.
Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS walisimamisha uanachama wa Ivory Coast katika jumuiya hiyo mwanzoni mwa mwezi Disemba baada ya kiongozi aliyemaliza muda wake wa nchi hiyo Laurent Gbagbo kung'ang'ania madaraka ya nchi licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumtangaza hasimu wake Alassane Ouattara kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwaka uliopita. Viongozi hao wametishia kutumia nguvu za kijeshi kumuondoa madarakani Gbagbo.
WARSHA YA UTEKELEZAJI KANUNI ZA UDHIBITI WA KEMIKALI
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwanza Dk Meshack Messi akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Issaria Mangalili na Meneja Maabara ya Mkemia Mkuu wa Kanda ya Ziwa Mara Baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Utekelezaji kanuni za udhibiti wa kemikali Zinazotobowa Tabaka la Ozon Uliofanyika Ukumbi wa BoT Mkowani Mwanza
Baadhi ya Washiriki wa Warsh Wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwanza,Dk.Meshack Messi wakatualipokuwa akifunguwa warshya Wasimamizi wa Sheria inayohusu Utekelezaji Kanuni za Udhibiti wa Kemikali zinazomongonyoa Tabaka la Ozon iliyofanyika kwenye Ukumbi wa BOT Mkowani Mwanza Jana{Picha na Ali Meja}
No comments:
Post a Comment