Wednesday, August 17, 2011

Mahakama Nchini Ukraine Yaamuru Tymoshenko Awekwe Kizuizini



Mahakama nchini Ukraine imetoa amri ya kumweka kizuzini Waziri Mkuu wa Zamani wa nchi hiyo Yulia Tymoshenko wakati kesi yake kuhusu mashtaka ya kutumia vibaya madaraka, ikiendelea.
Mwendesha mashtaka wa serikali aliomba Tymoshenko awekwe chini ya ulinzi wa polisi, akisema kwamba alikuwa akivuruga utaratibu wa mahakamani. Tymoshenko anatuhumiwa kuilazimisha kampuni ya taifa ya nishati Naftogaz kusaini makubaliano ya kununua gesi kutoka Urusi katika mwaka 2009. Tymoshenko anaekanusha mashtaka hayo, bado hakufungwa gerezani, lakini amepigwa marufuku kuondoka mji mkuu Kiev.

No comments:

Post a Comment