Wednesday, August 17, 2011

Waziri Wa Kwanza Mwanamke Wa Thailand Ameidhinishwa



Bunge la Thailand,limeidhinisha waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo.Yingluck Shinawatra wa chama cha Puea Thai alishinda kwa wingi mkubwa uchaguzi wa mwezi uliopita. Yeye ni dada wa Waziri Mkuu wa Zamani Thaksin Shinawatra, ambae anaishi uhamishoni kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya 2006.
Yungluck anasema kipaumbele chake ni kuwaunganisha wananchi. Changamoto kubwa inayomkabili kiongozi huyo mpya, ni kuziba pengo kati ya watu masikini na kundi la matajiri wa kijeshi na wafanyabiashara.

No comments:

Post a Comment